Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri wa Madini atoa siku 13 kumalizwa kwa mgogoro wa wachimbaji

Kiruswa Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa akizungumza na wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Ukombozi wakat

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa ametoa muda wa siku 13 kwa Uongozi wa wilaya ya Iramba na Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kumaliza mgogoro uliopo kwenye kitalu namba 22 unaosababishwa na wanachama na wadhamini wa mgodi wa Ukombozi kutokana na mgongano wa kimaslahi.

Dk. Kiruswa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi wa Ukombozi katika ziara yake ya siku moja ya kujitambulisha na kujionea baadhi ya miradi inayofanywa na wizara hiyo hasa katika sekta ya madini na kujua changamoto za wachimbaji.

Dk.Kiruswa Baada ya kusikiliza malalamiko ya pande zote mbili alisisitiza kuwa kama pande hizo hazitafikia makubaliano Serikali inaweza kufuta leseni hiyo na kutoa kwa mwekezaji mwingine ili uzalishaji uweze kuendelea.

" Natoa siku 13 kwa Uongozi wa wilaya ya Iramba na Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kumaliza mgogoro uliopo kwenye kitalu hicho katika machimbo ya Ukombozi vinginevyo Serkali inaweza kuifuta leseni hiyo" alisema Kiruswa.

Katika hatua nyingine Kiruswa aliupongeza Mkoa wa Singida hasa watendaji wa sekta ya madini kwa kuvuka malengo ya ukusanya wa maduhuli kwa mwaka huu wa fedha ambapo yalifikia asilimia 142.2 na kuwa hana mashaka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha mapato hayo yataongezeka kutokana na kufanya kazi vizuri.

Akijibu swali lililohusu wachimbaji wadogo kutopata leseni alisema kazi kubwa ya wizara kwanza ni kuwatambua,kujua idadi yao na wangapi wanaleseni kwani malengo la Serikali ni kusimamia sekta hiyo ya madini huku dhamira ni kuona kila mchimbaji anapata leseni na vifaa kama walivyoomba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live