Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri: Tanzania ina viwanda 61,110

6f54a533a417b5209d5582f22f1a751e Naibu Waziri: Tanzania ina viwanda 61,110

Wed, 3 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika ujenzi wa uchumi wa nchi na hasa katika kipindi hiki kwani viwanda vingi vinaanzishwa, kumilikiwa na kuendeshwa na wanawake.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonesho ya Bidhaa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi, Kigahe alisema “Nchi yetu kwa sasa ina takribani viwanda 61,110 ambavyo vimegawanyika katika viwanda vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo sana.”

“Kwa kipindi cha miaka mitano kutoka 2015 hadi 2020 jumla ya viwanda vipya 8,477 vilijengwa. Kati ya hivyo viwanda vikubwa ni 201, vya kati ni 460, vidogo ni 3,406 na vidogo sana ni 4,410.”

Alisema viwanda vingi vidogo na vya kati vinashughulika na uongezaji wa thamani mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo, misitu na maliasili zingine zinazopatikana kwa urahisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mercy Silla alisema maonesho hayo ni ya siku 10 kuanzia juzi kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.

Alitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni ‘Mwanamke na uwekezaji wenye tija kwa viwanda endelevu,’ lengo likiwa wanawake wanyanyukie kwenye hayo.

Alisema chama hicho kila mwaka kinawafikia wanawake 20,000 nchi nzima. Maonesho hayo yatafuatia na utoaji wa tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika kuanzisha biashara na viwanda.

Chanzo: habarileo.co.tz