Dodoma. Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula ameitaka Serikali kuangalia sekta ya uvuvi ili kuokoa viwanda vya kusindika samaki visife.
Mabula alikuwa akichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 bungeni jana Jumanne, Juni 18, 2019.
Amesema wanafahamu dhamira ya Serikali ya kuhakikisha viwanda vyote nchini vinapata nguvu, vijengwe kwa msingi wa uzalishaji na kutoa ajira.
“Mwanza tunaviwanda vya samaki vinane ama tisa, lakini ni viwanda vitatu ama vinne pekee ndivyo vinafanya kazi tena si kwa ufanisi unaotakiwa.
“Lipo tatizo kubwa baada ya operesheni (uvuvi haramu) Serikali ilikuja na bei elekezi ya samaki kuanzia Sh5,500 hadi Sh6,000,” amesema.
Hata hivyo, amesema leo hii kilo moja ya samaki inauzwa kwa bei ya Sh3,800 na kwamba, ili kumvua samaki anagharimu lita moja ya mafuta ambayo ni Sh2,800.
Pia Soma
- UCHOKOZI WA EDO: Kalamu na kamera havivuki ‘boda’ tena
- Maonyesho ya biashara ya sabasaba kuanza Juni 28
- Kesi mauaji ya Dk Mvungi yapata hakimu mwingine
- Wabunge wa CCM walalamikia Serikali kuchukua vyanzo vya halmashauri
Amesema kiwanda kimoja kilichokuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi 700 hivi sasa kinaajiri 50 hadi 90 kwa shifti moja na kilichokuwa na uwezo wa kupata tani 70, leo kinapata tani 10.
Mabula amesema wafanyabiashara wadogo wanapenda kuwepo kwenye sekta hiyo bali ni kwa sababu hakuna kazi za kufanya na ndiyo maana wanatafuta mitaji ya Sh200,000 ili waweze kuuza biashara yoyote na hivyo kujikimu na maisha.