Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NSSF, Wizara ya Mambo ya Nje wajadili uwekezaji vianja nje ya nchi

Katibu Mkuui NSSF, Wizara ya Mambo ya Nje wajadili uwekezaji vianja nje ya nchi

Sat, 9 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii - NSSF, Bw. Masha Mshomba tarehe 8 Julai 2022 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamejadili juu ya umuhimu wa kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na mfuko huo wa NSSF.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamezungumzia kuhusu uwekezaji kwenye viwanja vya Serikali nje ya nchi ili kuona namna ambavyo Wizara na NSSF wanaweza kushirikiana katika miradi ya ujenzi wa ofisi na vitega uchumi.

Aidha, Balozi Sokoine akaeleza kuwa Serikali ina miliki viwanja zaidi ya 40 kwenye maeneo ya uwakilishi nje ya nchi, hivyo akatoa rai kwa taasisi hiyo kushirikiana na Wizara katika kuviendeleza kwa kujenga majengo ya Ofisi za Balozi pamoja na vitega uchumi ili kuipunguzia Serikali gharama ya kupanga lakini zaidi kupata faida kutokana na vitega uchumi hivyo.

Naye Bw. Mshomba aliafiki wazo hilo la uwekezaji na kueleza kuwa NSSF imeshakuwa na mipango ya miradi ya uwekezaji nje ya nchi hivyo, wazo hilo limekuja wakati mwafaka na kwamba NSSF inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kufungua mipaka hususan katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Aidha, Kikao hicho kiliridhia kuundwa kwa timu ya Wataalamu kutoka katika pande zote mbili ili kuruhusu kufanyika kwa tathmini ya kina juu ya uwekezaji huo na faida zake ili kuweza kuwa na miradi ya pamoja na Wizara wenye tija kwa Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live