Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yawahimiza Walimu kuwekeza na kuchangamkia mikopo nafuu

0 34 NMB yawahimiza Walimu kuwekeza na kuchangamkia mikopo nafuu

Wed, 26 May 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Walimu wametakiwa kuwekeza na kujiendeleza katika kukopa mikopo nafuu yenye tija yakuweza kutatua  changamoto zinazowakabili ili kuweza kunufaika na kufurahia kazi wanayoifanya.



Akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella katika mafunzo ya walimu wa mkoani hapo  yaliyoandaliwa na Benki ya NMB ambaye ni Afisa elimu sekondari, Khalifani Omary alisema mafunzo hayo yatawajenga walimu katika kujiwekea kipato ili kuweza kujiendeleza kimaisha.

“Mafunzo haya yatawasaidia katika kuwaongezea elimu na kutoa fursa ya maoni namna wanavyoweza kunufaika na benki ya NMB ikiwa jitihada hizi zitaleta matokeo chanya nakuleta faraja kwa jamii,”alisema Omary.

Afisa elimu alisema jitihada hizo ni nzuri na zinaunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha watanzania waliowengi wanajumuhishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua vipato vyao na kiuchumi kwa ujumla hivyo anatoa rahi kwa taasisi nyingine za kifedha nchini kufanya jitihada hizo kama NMB. Alisema anashukuru huduma za kibenki zimeboreshwa na kusogezwa karibu na wateja wake kwani hapo awali walimu walipata taabu kutembea umbali mrefu hivyo benki ya NMB imekuwa chachu ya maendeleo katika jamii kwa kuwanufaika wateja wake.

Kwa upande wake Mkuu wa biashara za Kadi wa benki ya NMB, Philbert Casmir alisema wameandaa mafunzo yanayoitwa siku ya walimu ambapo wameanza mkoani Arusha kwa kutambua mchango wa mwalimu katika jamii na kutoa suluhisho ya changamoto zao katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mikopo nafuu na bima mbalimbali.

“Tunatambua mwalimu ni mwezeshaji katika jamii hivyo NMB tumekuja na muundo wa kutokutoa bidhaa au suluhisho ya maisha ya walimu kwani tunatambua kunachangamoto za ujenzi na kupitia mafunzo haya wataelimishwa nakuweza kutumia mikopo nafuu ya NMB kujiendeleza katika swala la ujenzi wa nyumba,”alisema Mkuu huyo.



Casmir alisema pia kuna bima za walimu na watanzania kwa ujumla zinazoweza kuwasaidia kupata fedha pamoja na hilo pia kunachangamoto ya elimu ya fedha watu kutoweka fedha katika taasisi za kibenki na kutunza majumbani hivyo elimu hiyo itawasaidia kufikisha ujumbe na faida za kuweka fedha benki katika jamii.

Baadhi ya walimu hao walisema wanashukuru benki ya NMB kwa kuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuwekeza fedha nakutumia katika matumizi sahihi ya kujiendeleza kiuchumi na kuwaletea maendeleo katika jamii.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Daraja mbili , Zukra Kalunde alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kufahamu umuhimu wa kadi pamoja na kujifunza namna ya kupata mikopo nafuu ya benki hiyo itakayowasadia kujiendeleza kiuchumi kama ujenzi wa nyumba zao za kuishi na biashara.
Chanzo: mtanzania.co.tz