Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yawa ya kwanza kutekeleza rasmi mpango wa ushirika afya

PM 1 NMB yawa ya kwanza kutekeleza rasmi mpango wa ushirika afya

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kupitia mpango wa Ushirika Afya, wanachama wa vyama hivyo watapewa mikopo isiyo na riba na Benki ya NMB kwa ajili ya gharama za matibabu kwa kutumia kadi za NHIF. 

Utiaji saini wa makubaliano hayo na vyama vya wakulima wa zao la tumbaku yanayouhusisha pia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulifanyika mkoani Tabora kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ushirika.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ndiyo aliyezindua rasmi mpango huo kwa kuwakabidhi kadi za NHIF wakulima wa tumbaku; Kulwa Mfaume, Saleh Mpemba na Athanas Semeduke ambazo ni miongoni mwa kadi 102 za kwanza ambazo zimetolewa na benki hiyo. Lakini pia kadi 90 zitatolewa kwa wakulima mkoani Kahama.

Vilevile, Majaliwa aliishukuru NMB kwa mchango wake wa kuviimarisha vyama vya ushirika na kuvifanya kuwa nguzo muhimu ya kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi alisema, NMB imetenga zaidi ya TZS bilioni 5 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima chini ya utaratibu wa Ushirika Afya. Lakini pia wana mpango wa kuongeza kiasi cha pesa ili kuwafiki wakulima zaidi ya 300,000 nchi nzima.

Utaratibu huu utarahisisha kazi ya kuwahamasisha wakulima kijiunga na vyama vya ushirika na utaongeza idadi ya watu wenye bima za afya kama serikali inavyotaka na kuelekeza.

Chanzo: ippmedia.com