Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yapata hadi ya 'Super brand'

NMB NMB NMB yapata hadi ya 'Super brand'

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya NMB imetunukiwa cheti cha kuwa ‘Superbrand’, na kuifanya kuwa benki pekee iliyopata hadhi hiyo nchini Tanzania mwaka huu.

Hadhi hiyo ya ‘Superbrands’ inatunukiwa chapa bora zaidi katika uwanja wao kufuatia mchakato mkali wa uteuzi na baraza la Superbrands na watumiaji wa bidhaa na huduma kutoka kote Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha amesema hadhi ya Superbrands ina maana kubwa kwa benki hiyo na kusisitiza kuwa cheti hicho ni chachu ya kuifanya benki yake kuwa chaguo kwa wateja wake.

"Hili lisingewezekana bila imani iliyopo kwa wateja wetu ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kwa miaka hii yote. Kama benki, tunafurahi kwamba wateja wetu wameweza kuamini chapa yetu na kuifanya kuwa miongoni mwa chapa bora Afrika Mashariki,” alisema.

Alibainisha kuwa benki hiyo imejipanga kuendelea kuongeza thamani kwa wadau wake wote wakiwemo wanahisa, wateja na jamii ambako benki hiyo inafanya kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live