Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yakabidhi vifaa vya milioni 30 - Nyanda za Juu

A7b6840852302b64868d691d740d4081.jpeg NMB yakabidhi vifaa vya milioni 30 - Nyanda za Juu

Sat, 18 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIFAA vyenye thamani ya Sh milioni 30 vimetolewa na Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu kuchangia huduma za kijamii katika maeneo ya Mkoa wa Songwe, Njombe na Mbeya.

Vifaa hivyo ambavyo ni vitanda vya wagonjwa na mashuka, bati na mbao za kuezekea na madawati vimeelekezwa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Lupila iliyopo wilayani Makete, Gereza la Wilaya ya Makete,Vituo vya Afya vya Ntaba na Isange vilivyopo Busokelo Wilayani Rungw mkoani Mbeya.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa katika maeneo na nyakati tofauti Meneja Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola alisema msaada huo ni sehemu ya faida itokanayo na Benki ya NMB ambayo hurejeshwa kwa kuihudumia jamii.

Wilayani Songwe, Mkoa wa Songwe NMB imechangia mabati 350 kwa shule ya msingi Kaloleni na zahanati ya Mamba na mkuu wa wilaya hiyo, Samwel Jeremiah alisema Benki ya NMB imeendelea kuwa wadau wakubwa wa maendeleo katika sekta ya elimu afya na majanga.

Katika wilaya ya Makete, mkoa wa Njombe Benki ya NMB imechangia mabati kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kupumzikia mahabusu Gereza la Wilaya na madawati katikaa shule ya Sekondari Lupila na Mkuu wa wilaya Makete Veronica Kessy alisema uwepo wa Benki hiyo nchini ni mkombozi wa huduma zote za kijamii.

Katika wilaya ya Rungwe, Halmashauri ya Busokelo, Mkoani Mbeya Benki ya NMB imetoa msaada wa vitanda 10 vya wagonja na vitanda viwili vya kujifungulia wanawake wajawazito na mashuka kwa vituo vya afya Ntaba na Isange.

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Julius Chalya alisema Benki hiyo imekuwa na misaada endelevu kulingana na mahitaji ya kielimu, afya na majanga na hivyo kurahisisha huduma za kijamii ni vyema wananchi wakaendelea kuiunga mkono Benki hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz