Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB yaipiga jeki Sekondari ya Jambiani

E0f967f310f7c9e3a5bfe89bc83af164 NMB yaipiga jeki Sekondari ya Jambiani

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BENKI ya NMB, Tawi la Zanzibar imekabidhi mabati 200 na vifaa vingine vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari ya Jambiani, Kusini Unguja.

Akizungumza katika hafla ya makabidhianao hayo iliyofanyika shuleni hapo jana, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuimarisha sekta ya elimu.

“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana pamoja na jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200 kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua,”alisema Donartus.

Alisema elimu ni kichocheo cha maendeleo, hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata elimu na kusisitiza kuwa, ndiyo maana NMB imeamua kuisaidia shule hiyo.

Mwakilishi wa Jimbo la Paje ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Uvuvi, Mifugo na Umwagiliaji, Sudi Nahoda, ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kusema utasaidia kutatua changamoto ya kuvuja kwa shule hiyo.

“Tunawahakikishia kuwa, msaada huu mliotupatia una thamani kubwa na kiuhalisia, NMB ni moja kati ya mashirika yanayojali jamii katika kuleta maendeleo,”alisema Nahoda.

Kaimu Mkuu wa Shule ya Jambiani, Haji Haji ameishukuru NMB kwa msaada huo na kuongeza kuwa, kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliwa na ubovu wa madarasa hali uinayowafanya wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo katika vipindi vya mvua.

Chanzo: habarileo.co.tz