Hadi sasa programu hiyo iliyoanza miaka 13 iliyopita imezalisha wataalamu wa maswala ya kifedha na kibenki zaidi ya 60.
Wanufaika nane wa uwekezaji huo walihitimu hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu.
“Ndoto zetu za kuwa wataalamu wa masuala ya kibenki leo imetimia. Tunaahidi kufanya kazi kwa nguvu zetu zote kama waajiriwa wa taasisi bora na kubwa ya fedha nchini Tanzania,” Amanda Eseko alisema kwa niaba ya wenzake.
Aliongeza kuwa: "Miaka miwili ya mafunzo mbalimbali waliyopitia haikuwa ya lelemama. Hata hivyo, alifafanua, miaka hiyo imekuwa ya manufaa makubwa kwao kwasababu wamejifunza mambo mengi na kupata fursa ya kufanya kazi NMB na kulihudumia taifa kwa ujumla," alisema.
Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB, Emmanuel Akonaay, alisema ana matumaini makubwa sana na vijana hao ambao hana shaka wataisaidia benki hiyo kuendelea kuwa kinara wa huduma za kifedha nchini.
“Kwa kipindi chote cha mafunzo yao, hawa vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu. Hii ni pamoja na kuweza kupata amana zenye thamani ya Sh. bilioni 7 na kusaidia kufunguliwa kwa akaunti mpya 5,000,” alisema Akonaay
Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa Bodi wa NMB, Ramadhani Mwikalo, alisema kuwa uendelezaji wa vipaji kama huo ni moja ya vitu vinavyofanya NMB kuwa mwajiri bora na kinara nchini, na kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi mkubwa, ndiyo rasilimali namba moja ya benki hiyo na mtaji unayoifanya kuongoza sokoni.
Awali, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Filbert Mponzi, aliwaambia wahitimu hao kuwa kuajiriwa na mwajiri bora Tanzania ni kuwa sehemu sahihi na katika mikono salama kiajira.
Ili wafanikishe, alibainisha, ni lazima wazingatie kupata matokeo chanya katika kila wanalolifanya kwani hiyo ndiyo siri ya kufanikiwa kwa watu kama yeye ambao walianzia ngazi za chini walipoajiriwa NMB.