Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB wazindua 'NMB Loan'

NMB NMB NMB wazindua 'NMB Loan'

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya NMB imezindua huduma ya mikopo ya elimu ya juu iitwayo ‘NMB Elimu Loan’ na kuitengea kiasi cha Shilingi Bilioni 200 za Kitanzania kwa ajili ya kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa riba nafuu maalum kwaajili ya Watumishi na Wafanyakazi ambao mishahara yao inapitia kwenye Benki hiyo.

Taarifa ya NMB kwa Vyombo vya Habari imesema Mtu yeyote anaweza kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu ama kwaajili ya Vijana, Watoto au Wenza.

Maelezo ya ziada ya mkopo huo ni kama ifuatavyo, mkopo unatolewa kwa Mwajiriwa yoyote ambae ni Mteja wa NMB, unaanzia TZS 200,000 hadi TZS milioni 10 kwa mwaka kwa Mtu mmoja na riba yake ni 9% na muda wa marejesho wa miezi 12 ambapo unatolewa pia kwa ngazi ya Vyuo vya kati vikiwemo Vyuo vya Ufundi.

Akitangaza kuanzishwa kwake rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema yafuatayo ““Huu ni utekelezaji wa makubaliano yetu na Wizara ya Elimu ya kuanza kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kupunguza utegemezi wa Waajiriwa kwa Bodi ya mikopo (HESLB) pale wanapotaka kujiendeleza kimasomo na pia kuwalipia ada vijana wao”.

Kwa kuanzisha huduma hii ambayo inapatikana kwenye tawi lolote la Benki hii, NMB inakuwa imetimiza ahadi iliyoitoa mwaka 2022 ya kuisaidia Serikali kuipunguzia HESLB mzigo wa kufadhili masomo ya juu na kuwa na vyanzo vipya vya mikopo ya elimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live