Benki ya NMB Bank Plc imeibuka Mshindi wa jumla Kitaifa kama Mlipa Kodi Mkubwa zaidi Tanzania na kama Mlipa kodi bora zaidi anayelipa kodi kwa hiari (Most Compliant Tax Payer) katika Tuzo zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) November 24 Dar es salaam.
Ukiwa huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Benki ya NMB kupata tuzo hizi, jumla ya Tuzo ilizopata ni Mshindi wa jumla Kitaifa yaani Taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (sekta zote).
Mshindi wa Jumla Kitaifa: Taasisi Bora inayolipa kodi kwa hiari kwa kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer).
Mshindi wa kwanza: Mlipa Kodi mkubwa zaidi katika kundi la Taasisi za Fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo) ambapo akiongea baada ya kupokea Tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna alisema tuzo hizo ni matokeo chanya ya misingi imara ya utawala bora na uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa Wateja.
“Nawashukuru Wateja wetu na Watanzania wote kwa kuendelea kuiamini Benki ya NMB kama Mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao, naishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya Biashara nchini na kipekee nawashukuru Wafanyakazi wenzangu wote wa Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa ujumla”
Tuzo hizo za Mamlaka ya Mapato Tanzania zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko.