Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB, NBC kuunga mkono ajenda ya uchumi wa Buluu

Uchumi Wa Buluu NMB, NBC kuunga mkono ajenda ya uchumi wa Buluu

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki za NMB na NBC, zimejipanga kuendelea kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa ajenda ya Uchumi wa Buluu kupitia utoaji wa huduma bora za kibenki ninazokidhi matakwa ya wananchi.

Benki za NMB na NBC, zimejipanga kuendelea kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa ajenda ya Uchumi wa Buluu kupitia utoaji wa huduma bora za kibenki ninazokidhi matakwa ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na viongozi wa taasisi hizo, baada ya kuandika historia mpya visiwani humo kwa kutoa mkopo wa pamoja wa Sh470 bilioni unalenga kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024. Mkopo huo wa aina yake, Benki ya NBC ilichukua nafasi ya Mwekezaji Mkuu huku benki ya NMB ikiwa mfadhili mwenza wa mkopo huo ambao Serikali ya Zanzibar italazimika kurejesha ndani ya kipindi cha miaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali yake imepanga kutekeleza miradi ya maendeleo mara mbili mwaka huu ukilinganisha na miradi iliyotekelezwa mwaka uliopita kutokana na upatikanaji wa mkopo huo. Amesema Serikali yake tayari imeweka mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa fedha za mkopo huo zinarejeshwa ndani ya kipindi cha miaka nane kama ilivyopangawa na kuwatoa hofu wote wenye wasiwasi juu ya Serikali yake katika la ulipaji. “Leo tumeandika historia mpya kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa benki za ndani kutoa mkopo kwa Serikali yetu. Baada ya upatikanaji wa hizi fedha tumepanga kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesema Dk Mwinyi. Akizungumza baada ya utiaji saini wa mikataba ya mkopo huo katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar, Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Juma Kimori ameutaja mkopo huo kuwa wa kihistoria katika sekta ya benki na fedha nchini. “Tuna heshima kubwa kuwa sehemu ya mkopo huu unaolenga kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ushiriki wetu katika mkopo huu unadhihirisha dhamira ya dhati ya kusaidia maendeleo na ustawi wa jamii visiwani Zanzibar,” Kimori amesema. Kimori ameongeza, “Tunaamini mkopo huu utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii na kuchangia ukuaji wa maendeleo endelevu ya uchumi hivyo kuleta manufaa ya kudumu kwa wananchi.” Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi amesema mkopo huo akisisitiza kwamba utasaidia katika kufikia dira ya Serikali ya Zanzibar ya ukuaji wa uchumi jumuishi na upatikanaji wa maendeleo endelevu. Sabi ameongeza kuwa mpangilio wa mikopo unaashiria mafanikio makubwa na utasaidia kufikia malengo ya pamoja ya uwezeshaji wa jamii, ushirikishwaji na kusisitiza kuwa utaimarisha ustawi wa watu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Saada Mkuya amesema fedha hizo zitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za kijamii ikiwa ni utekelezaji wa dira ya Maendelo ya Serikali hiyo ya Mwaka 2020/2026 inayolenga kuboresha miradi yab elimu, afya, miundombinu, maji na ujenzi wa viwanja vya michezo. "Tulifanya mazungumzo na benki zote za ndani katika harakati za kupata vyanzo mbadala vya fedha na tunafurahi kwamba benki za NMB na NBC zilionyesha nia kuanzia mwanzoni. Tunafurahi kwamba leo tumesaini mikataba ya mkopo na benki hizi baada ya mazungumzo ambayo yamechukua karibu miezi na tunaamini huu ni mwanzo tu,” amesema Dk Mkuya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live