Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB, Mastercard wazindua kadi za kisasa

C3fafb82805858c1b2ba8d2c30f4a726.png NMB, Mastercard wazindua kadi za kisasa

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni ya Mastercard imezindua matumizi ya kadi za kisasa zaidi za kielektroniki zitakazokuwa chachu ya mapinduzi ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha.

Kadi hizo zinazowezesha malipo ya kabla na malipo kwa mkopo, zilizinduliwa jijini Dar es Salaam juzi katika hafla iliyoshuhudiwa na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk Bernard Kibesse.

Kwa mujibu wa viongozi wa benki hiyo, ushirikiano na Mastercard kutoa huduma hizo mbili utakuwa wa manufaa si kwa wateja wa NMB pekee, tu bali pia kwa sekta ya ifedha na Watanzania kwa jumla.

Hiyo inatokana na kadi hizo kuweza kutumiwa na wateja na wasio wateja wa taasisi hiyo ya kifedha.

Katika mkakati wake wa kutoa huduma kupitia kadi za kielektroniki za Mastercard zenye uwezo wa kutunza fedha na kufanya malipo kwa intaneti au katika manunuzi (POS), NMB imepanga kuzisambaza kwa zaidi ya watu milioni tatu ndani ya miaka mitano.

Dk Kibesse aliyekuwa mgeni rasmi alisema litakuwa jambo jema kama lengo hilo litakuwa maradufu ili huduma hiyo mpya ichangie kuwapo uhakika wa Watanzania wengi kuwa na huduma za kibenki muda wote na mahali popote.

Alisisitiza kadi hizo kusambazwa hadi vijijini na maeneo ya pembezoni ili kuwasaidia wakulima kujiwekea akiba hata kabla ya kufungua akaunti. Alisema hilo likifanikiwa, Tanzania itakuwa imepiga hatua katika jitihada zake za kuwa na uchumi usiotegemea malipo ya fedha taslimu.

“Sekta ya benki leo tena inashuhudia mapinduzi makubwa hususani kuhakikisha Tanzania inapiga hatua katika matumizi ya kadi na kutupeleka katika nyanja za kimataifa ambapo Watanzania watafanya miamala yao hasa malipo, kupitia kadi hizo za kisasa kabisa,” alisema Dk Kibesse.

“NMB, pelekeni huduma hii kwa Watanzania hasa wa vijijini ambako wengi ni wakulima kwani hii itakuwa ni suluhisho kubwa kwao kujiwekea akiba hata kabla hawajafungua akaunti,” alisema

Chanzo: habarileo.co.tz