Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB MastaBata yatoa washindi 384

544eaa83677557479b70857ba8adcee4 NMB MastaBata yatoa washindi 384

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPENI ya NMB MastaBata inayoendeshwa na Benki ya NMB ikilenga kuhamasisha matumizi ya kadi za mastercard, masterpass QR na POS, imetoa jumla ya washindi 384 walioshinda fedha taslimu na zawadi zenye thamani ya Sh milioni 93.6.

NMB MastaBata iliyoanza Novemba 24, mwaka jana inawazawadia fedha taslimu Sh 100,000 washindi 40 wa kila wiki, huku ikitoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 2.4 kwa washindi wa mwezi na washindi wa droo kuu watagharamiwa ziara ya utalii wa ndani.

Akizungumza wakati wa droo ya tisa ya kila wiki jana jijini Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa NMB, Manfred Kayala alisema droo tisa za kila wiki zimezalisha washindi 360 walioshinda fedha taslimu, huku droo za kila mwezi zikitoa washindi 24 waliojishindia zawadi mbalimbali.

“Kupitia droo za kila wiki tumewapata jumla ya washindi 360 waliojishindia pesa taslimu Sh milioni 36), huku droo mbili za kila mwezi tukizalisha washindi 24 yaani 12 kwa kila mwezi ambao wameshinda zawadi mbalimbali zenye thamani ya Sh miliono 57.6),” alisema.

Kayala aliwataka wateja wa NMB kuendelea kufanya manunuzi na malipo yao kupitia NMB mastercard, masterpass QR na POS ili kujiongezea nafasi za kushinda droo chache zilizobaki ikiwamo kuu ya mwisho.

Alisema ukiondoa Sh 100,000 wanazovuna washindi 40 wa kila wiki, droo za mwezi huwapa washindi zawadi zenye thamani ya Sh milioni 2.4 zilizogawanywa katika makundi matatu, kundi la kwanza likiwa na zawadi ya simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20 yenye thamani hiyo.

Kundi la pili lenye zawadi zenye thamani hiyo linajumuisha zawadi za friji dogo, mashine ya maji ya kunywa, jiko la kisasa la kupashia vyakula moto na simu aina ya Samsung A21, huku kundi la tatu likiwa na runinga iliyolipiwa DSTv miezi mitatu, kompyuta mpakato na simu ya Samsung A21.

Kayala alisema washindi wa droo inayotoa zawadi ya ziara ya utalii wa ndani katika hifadhi za Serengeti, Ngorongoro ama visiwa vya Zanzibar, watakuwa huru kuchagua zawadi mbadala zenye thamani ya Sh milioni nane kwa kila mmoja.

Chanzo: habarileo.co.tz