Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB MastaBATA yamwaga mil 56.8/-

A720ac46c2048db6491df1bfb1caff0a.png NMB MastaBATA yamwaga mil 56.8/-

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

ZAWADI za jumla ya Sh milioni 56.8 zimenyakuliwa na washindi wa droo ya NMB MastaBATA.

NMB MastaBATA ni kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, mwaka jana na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambapo zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo fedha, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro kwa washindi.

Hadi jana jumla ya washindi 280 wa kila wiki wamepatikana ambapo kila mmoja ameshinda Sh 100,000 tangu kuanza kwa shindano hilo.

Aidha, jana walipatikana washindi 40 wa kila wiki waliojinyakulisha Sh 100,000 kila mmoja na kufanya idadi ya washindi hao kufikia 280.

Katika droo hiyo ya saba iliyosimamiwa na Pendo Albert kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), kigezo cha ushiriki ni matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR na NMB MastaBATA imewazawadia jumla ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi wakiwa wamejishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20 yenye thamani ya Sh milioni 2.4.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Biashara ya Kadi ya NMB, Yusuph Achayo alisema jana ilikuwa ni droo ya saba iliyotoa zawadi za jumla ya Sh milioni nne, ambapo Sh 100,000 zilitolewa kwa washindi 40.

Zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, jokofu, laptop, simu (Samsung A70), water dispenser na microwave.

Chanzo: habarileo.co.tz