Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB Kukuza makusanyo ya mapato ya Utalii Zanzibar

NMB ZNZ.jpeg Zoezi zima la mkataba likihitimishwa

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya NMB imesaini makubaliano ya kimkakati na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikiana katika kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya utalii visiwani humo kupitia mifumo ya kidijitali.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk Khamis.

Kupitia ushirikiano huu, Benki ya NMB itachagiza shughuli za kitalii kupitia;

ambapo itawekeza kwenye mfumo wa kidigitali utakaotumika kufanya makusanyo ya Serikali katika vituo vyote vya utalii Zanzibar

Itasambaza mashine za malipo (POS) kwenye vituo vya makusanyo na vivutio vya utalii. Hii itawawezesha watalii kulipia ada na tozo zote kupitia kadi zao za Mastercard, Visa na UnionPay

Pia itatoa elimu na kuhamasisha watu kuzidi kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo visiwani humo kupitia matamasha na promosheni mbali mbali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live