Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NMB, Halotel kutoa huduma ya Tehama shule 200 za serikali

9587 Nmb+pic TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya NMB na kampuni ya mawasiliano ya Halotel zimeingia mkataba wa makubaliano ya miaka miwili ya kutoa huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika shule za Serikali zaidi ya 200 hapa nchini.

Wakati wa makubaliano hayo yaliyoshuhudiwa  leo Agosti mosi mbele ya waandishi wa habari na mwaka wa kwanza NMB itatoa kompyuta 350 kwa shule 100 na jukumu la Halotel litakuwa ni kuziunganisha na huduma ya intaneti.

Katika kuzipata shule hizo Serikali itashirikiana na Wizara ya tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) na wizara ya Elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker amesema kwa kushirikiana na Halotel kila shule ambayo NMB itatoa kompyuta Halotel watatoa huduma ya intaneti ina mahali ambapo Halotel watataka kupeleka Inteneti NMB itatoa kompyuta.

“Tunataka kusaidia taifa hili kuwa na watu wenye weledi hususan masuala ya Tehama, bila kuwa na watu wengi wenye weledi hata biashara zetu haziwezi kufanyika. Mtu akiunganishwa na intaneti anakuwa ameunganishwa na dunia,” amesema Bussemaker.

Upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Van Son amesema wao wako tayari kushirikiana na wadau wote wa maendeleo ya elimu nchini.

“Wadau wengine waje sisi tuko tayari kushurukuana nao kadri tutakavyoweza kwani tunatamani sana kuwekeza katika kuwainua watanzania,” amesema Son.

Hata hivyo sio mara ya kwanza kwa NMB kutoa kompyuta katika shule kwani tayari imetoa kompyuta zaidi ya 600 katika shule mbalimbali na halotel tayari wamekwisha unganisha zaidi ya kompyuta 417. Lakini ni kwa mara ya kwanza kushirikiana.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz