Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NIC yazindua Bima Kubwa ya Flex

C6dcbd64c040d325db09e8fba35f7e4f.jpeg NIC yazindua Bima Kubwa ya Flex

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Taifa la Bima (NIC) limezindua bidhaa mpya ya Bima kubwa ya Flex ambayo itatoa fursa kwa taasisi au kikundi kukata bima hiyo kwa kulipa kidogo kidogo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dk Elirehema Dorie amesema bima hiyo ina faida kubwa kwa wenye magari katika taasisi, kampuni au kikundi kwa kuzingatia mahitaji yote wakati gari inapopata ajali.

Dorie amesema Bima ya Flex inatoa nafasi ya kulipa hadi mtu wa tatu katika ajali pamoja na kulipa majeruhi.

Amesema bima hiyo kwa wateja wake wakati gari ikiwa imepata ajali ikiwa matengenezo mteja atalipwa Sh 50,000 kwa wiki tatu ambapo gari litakuwa tayari limeshatengenezwa.

Dorie amesema kuwa ulipaji wa Bima hiyo kidogo kidogo hakuna riba watakayotoza lengo ni kuona wateja hawapati usumbufu.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Shirika limeamua kubadilika kwa kwenda kasi na Mipango ya Serikali kwa baada ya miaka 10 ijayo asilimia 50 watanzania wawe na bima.

Amesema kuwa Shirika litaendelea kutoa elimu ya Bima kwa njia yeyote lengo ni kutaka watanzania wawe na uelewa bima katika kutatua changamoto zao.

Amesema wataendelea kutoa bidhaa mbalimbali za Bima kwa kila eneo kutokana wao wabobezi katika eneo hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz