Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NIC yaanzisha bima ya mazao kwa wakulima

69673 Pic+bima

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bariadi. Serikali ya Tanzania imezindua bima ya mazao itakayowafidia hasara watakayopata wakulima kutokana na  ukame, uharibifu na uvamizi wa wadudu na mafuriko.

Hafla ya uzinduzi  huo imefanyika leo Jumamosi Agosti 3, 2019 katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu yanakofanyika maonesho ya  Nanenane kitaifa.

Akizindua bima hiyo Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga ametaja majanga mengine yatakayofidiwa kwa bima hiyo inayotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) i uharibifu wa mazao unaotokana na upepo mkali, uvamizi wa wanyamapori, moto, tetemeko la ardhi na radi.

Bima hiyo itahusisha mazao yote na itatolewa kwa wakulima wote nchini lakini kwa kuanzia itahusisha mazao ya kimkakati ambayo ni pamba, kahawa, korosho, mpunga, mahindi na tumbaku.

"Tutaanza na zao la pamba katika mkoa wa Simiyu kama Mkoa wa mfano. Baadaye tutahamia kwenye kahawa mkoani Kagera. Lengo letu hadi mwakani tuwe tumefikia mazao matano," amesema Hasunga.

Akizungumzia  sababu za kuanzishwa kwa bima hiyo, mkurugenzi mkuu wa NIC, Profesa Elirehema Dorie amesema lengo ni kuhakikisha sekta ya kilimo anayoajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania inasaidia  kufikia utekelezaji wa mkakati wa kuwa na Taifa lenye uchumi wa kati kupitia maendeleo ya sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Pia Soma

"Bima hii itawakwamua wakulima kwa kuwapatia kinga dhidi ya uharibifu wa mazao yao yanapokuwa shambani," amesema Profesa Dorie.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametumia uzinduzi huo kumhakikishia Waziri Hasunga na Profesa Dorie utayari wa wakulima wa Mkoa huo  kupokea na kutumia bima ya mazao.

"Simiyu tayari tuna kanzi data ya wakulima wote inayoonyesha aina ya mazao yao, hekari wanazolima na makadirio ya mavuno. Tuko tayari kuwa Mkoa wa mfano kutekeleza mpango huu wa Bima ya mazao," amesema Mtaka.

Chanzo: mwananchi.co.tz