Umoja wa machinga mkoa wa Dar es Salam umeiomba Serikali kufanya mazungumzo na Shirika la Nyumba la Taifa NHC, kwa ajili ya uwekezaji kwa baadhi ya miradi yake ili kuinua uchumi wa taifa.
Akisoma risala mbele ya Rais Samia, Mwenyekiti wa Machinga, Bw. Yusuph amesema kuwa baadhi ya maeneo yanayomilikiwa na NHC ni mazuri kwa kufanyia biashara.
Akifafanua suala hilo Bw. Yusuph amesema kuwa NHC inaweza kujenga maduka makubwa ya kisasa 'mall' kwa ajili ya machinga kufanyia biashara zao jambo amablo litapunguza mrundikano wa machinga pembezoni mwa mji.
Aidha wameomba Serikali kuwashirika kwenye mipango ya ujenzi wa masoko ili waweze kusaidia kwenye uchaguzi wa maeneo yenye tija kibiashara kuliko kujenga na kulazimisha machinga kuhamia maeneo yasiyo na maslahi.