Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHC kumekucha mradi wa nyumba 5,000

3b1073428f4055fa4a45054c330054b9 NHC kumekucha mradi wa nyumba 5,000

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), linatarajia kutumia zaidi ya Sh bilioni 413 kutekeleza vipaumbele mbalimbali, ikiwemo utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 5000 za gharama ya kati ujulikanao kama Samia Housing Scheme.

Hayo yamebainishwa na Meneja Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 9, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji na muelekeo wa shirika hilo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Seguya amesema kuwa mradi huo pekee utaweza kutoa ajira kwa Watanzania 26,400, ajira za moja kwa moja zikiwa 17,600 huku zile zisizo za moja kwa moja zitakuwa 8,800.

Ameongeza kuwa asilimia 50 ya mradi huo wa Samia Housing Scheme utatekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, huku Mkoa wa Dodoma utatekelezwa kwa asilimia 20 na mikoa mingine ambayo hakuianinisha utatekelezwa kwa asilimia 30.

“Nyumba hizi zitaanza kujengwa mwezi Septemba eneo la Kawe, Dar es Salaam (nyumba 500) na Medeli jijini Dodoma (nyumba 100),” amesema Saguya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live