Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHC kukusanya Sh10 milioni kwa mwezi mpaka wa Mtukula

Nhcpicx Data Makamu wa Rais akizindua majengo ya NHC Mutukula, Kagera

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kuingiza kiasi cha Sh10 milioni kwa mwezi kutokana na ujenzi wa jengo la biashara la Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo,  Nehemia Mchechu ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya  ujenzi katika mradi huo ambao umegharimu Sh3.1 bilioni.

Amesema lengo la NHC ni kujenga masoko maeneo ya mpakani na yote kuyapedezesha hivyo baada ya kukamilisha ujenzi wa Mtukula wataanza ujenzi kituo cha pamoja katika mpaka wa Irola - Roliya.

"Jengo letu la Mtukula lilianza kujengwa Desemba, 31, 2014 tayari limekamilika lina sehemu 42 za biashara, sehemu 36 zimeishapangishwa kwa ajili ya biashara," amesema Mchechu.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Philip Mpango amelitaka shirika hilo kujenga nyumba zenye ubora na watoze bei nafuu Ili wafanyabiashara wasije kukimbilia upande wa pili wa nchi ya Uganda.

"Hakikisheni miradi ya ujenzi inajengwa kwa ubora Ili Mtukula na kwingineko mipakani kuendelee kun'gara pia angalieni mnapojenga kwa ajili ya makazi Ili baada ya miaka mitano pasionekane ni makazi horela wakati pamepimwa," amesema Dk Mpango.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live