Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NFRA yanunua tani 175,000 za nafaka

Maguni Ya Mahindi NFRA yanunua tani 175,000 za nafaka

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), imepanga kununua tani za nafaka 305,000, ambapo hadi kufikia Septemba 5, 2023 tayari ilinunua tani za nafaka 175,000.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 8, 2023, wakati akiahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge ulioanza Agosti 29, 2023. - “Naomba nizungumzie hali ya masoko yaliyovunwa msimu wa mwaka 2022/23. Katika kuhakikisha mazao yaliyovunwa msimu wa mwaka 2022/2023, yanapata soko la uhakika, bei nzuri na nchi kuwa na uhakika wa usalama wa chakula.

“Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imepanga kununua tani 305,000 za nafaka, hadi kufikia Septemba 5, 2023, tani 175, 000 sawa na asilimia 57 za lengo zimeshanunuliwa,” amesema Waziri Mkuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live