Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NFRA kuingia ubia na wafanyabiashara, wakulima

Mazao NFRA kuingia ubia na wafanyabiashara, wakulima

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umesema unakusudia kuingia mikataba ya ununuzi wa nafaka “framework agreement” kati yake na wakulima na wafanyabiashara ili kuongeza wigo wa kufikia ununuzi wa tani 700,000 za mahindi meupe na mpunga kwa msimu wa 2024/25.

Afi sa Mtendaji Mkuu, Dk. Andrew Komba amesema katika taarifa iliyochapishwa leo, Machi 30 na gazeti la HabariLEO kuwa NFRA inakusudia kuanza kununua nafaka kuanzia Julai 1, ununuzi utakaofanyika kupitia maghala ya kikanda.

“Ununuzi huo utafanyika kwenye maghala yaliyopo kanda za Arusha (ghala la Arusha na Babati), Dodoma (ghala la Dodoma na Manyoni), Kipawa (Dar es Salaam), Makambako, Songwe, Shinyanga, Songea na Sumbawanga (Sumbawanga na Mpanda) na vituo vingine ambavyo vitafunguliwa na Wakala,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, NFRA imeweka wazi sifa za wakulima watakao nufaika na mpango huo kuwa ni wale ambao wana shamba kuanzia ekari 100 katika eneo moja na kuwepo na uthibitisho huo kutoka Serikali ya Kijiji/ Halmashauri ya Wilaya.

“Vilevile, Mkulima awe na uwezo wa kuzalisha kuanzia tani 200 za Mahindi Meupe au Mpunga,” imeongeza taarifa hiyo.

Kwa mfanyabiashara, NFRA inalenga ambaye ana uwezo wa kuiuzia NFRA kuanzia tani 2,000 hadi 5,000 za Mahindi Meupe au Mpunga. Awe na Hati hai ya kutodaiwa kodi (valid tax clearance), na pia Mwombaji anaelekezwa kuwasilisha barua ya maombi ya kuiuzia NFRA Mpunga au Mahindi Meupe kabla au ifikapo tarehe 20 Aprili, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live