Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NFRA ilivyobanwa malipo ya wauza mazao

Chakula Nafaka NFRA ilivyobanwa malipo ya wauza mazao

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dk Hussein Mohamed Omar ameuagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuhakikisha malipo ya wakulima na wafanyabiashara wa mazao wanaouzia wakala huo yanafanyika ndani ya saa 72 baada ya kupokea mazao yao na kuhakiki malipo.

Dk Omar ametoa agizo hilo jana alipotembelea wakala huo uliopo Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Kituo hicho kinaendelea na msimu mpya ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima kwa bei ya Sh 700 kwa kilo 1 kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu amezungumza na baadhi ya wakulima wauzaji wa mazao ambao licha ya kufurahishwa na kasi ya kituo hicho kupokea na kupima mazao walilalamikia ucheleweshaji wa malipo.

Ametoa maelekezo matatu kwa ofisa mtendaji mkuu wa NFRA ya kuhakikisha malipo yanafanyika ndani ya siku tatu tangu mkulima au mfanyabiashara alipofikisha mazao yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live