Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEMC yashiriki maonesho Qatar

Maonesho Qatar NEMC (600 X 351) NEMC yashiriki maonesho Qatar

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar, ili kutoa elimu na kuonesha namna mazingira ya uwekezaji yalivyoboreshwa na kurahisishwa kwa ajili kuvutia uwekezaji.

Watendaji wa NEMC walioshiriki maonesho hayo wameelezea fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania hasa katika kilimo kinachozingatia uhifadhi wa mazingira pamoja na utalii.

Baraza hilo la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira pia limewaelimisha wawekezaji wa Kimataifa juu ya kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live