Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEMC yakamata shehena ya gunia 8 za mifuko ya plastiki Mwanza

82921 Nemc+pic NEMC yakamata shehena ya gunia 8 za mifuko ya plastiki Mwanza

Thu, 7 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza wamekamata shehena ya mifuko isiyokidhi viwango gunia 8 yenye thamani ya Sh10 milioni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Lulu Mussa imeeleza kuwa mifuko hiyo iliingizwa jijini Mwanza kupitia bandari bubu ya Bwiru ikitokea nchi jirani. Mkuu huyo ameeleza kuwa shehena hiyo ilikamatwa Novemba 4 mwaka huu 2019, baada ya baraza hilo kupitia kikosi kazi cha kitaifa cha kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kufanya operesheni nchi nzima ka lengo la kusaka mifuko hiyo isiyokidhi viwango. Aidha, Lulu Mussa amesema kuwa Oktoba 30, mwaka huu 2019 NEMC pia ilikamata marobota 21, katika wilaya za Misenyi mkoani Kagera na marobota saba mkoani Arusha ambayo yanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Arusha huku upelelezi wa mashauri hayo ukiwa unaendelea. Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa wito kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko mbadala kuhakikisha wanazingatia matakwa ya sheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz