Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NCC kutoa mchanguno bei vifaa vya ujenzi

Vifaa Ujenzi NCC kutoa mchanguno bei vifaa vya ujenzi

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limekusudia kuanza kutoa fahirisi za bei za vifaa na ujira katika shughuli za ujenzi kila mwezi.

Pia iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mwongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchini kwa kuandaa gharama za msingi za wakandarasi. Haya yalibainishwa na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo jijini hapa jana, Dk Matiko Mtuki wakati wa kuelezea utekelezaji wa majukumu ya baraza.

Alisema katika shughuli zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka 2022/23 ni kutoa fahirisi za bei za vifaa, mitambo na ujira katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kusomesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi.

“Hadi kufika Januari 31 mwaka huu baraza limekusanya takwimu, kuchakata na kutoa fahirisi za bei za vifaa vya ujenzi kwa kila mwezi.” Dk Mtuli alisema pia iko katika hatua za kukamilisha mwongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchini kwa kuandaa gharama za msingi za mkandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara kwa kila mikoa ya Tanzania Bara.

Alisema mikakati iliyopo ni kuhakikisha kuwa mwongozo huo unatumika mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live