Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBS: Mfumuko wa bei umepanda nchini

Bei Ya Vyakula NBS: Mfumuko wa bei umepanda

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioisha mwezi January, 2023 umeongezeka hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia mwezi December, 2022, hii ikimaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mezi January, 2023 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi December, 2022.

“Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi January, 2023 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi January, 2023 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi December, 2022”

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi January, 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi December, 2022 ni pamoja na ngano (kutoka 6.0% hadi 7.7%), unga wa mtama (kutoka 1.0% hadi 3.9%), samaki (kutoka 4.2% hadi 4.3%), matunda (kutoka 1.9% hadi 5.5%), mbogamboga (kutoka 3.6% hadi 5.2%), viazi vitamu (kutoka 3.9% hadi 5.3%), choroko (kutoka 1.3% hadi 5.6%) na kunde (kutoka 8.7% hadi 13.9%).

Kwa upande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei ni pamoja na nguo za wanawake (kutoka 2.6% hadi 2.7%), viatu vya Wanawake (kutoka 3.4% hadi 3.5%), vifaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani kutoka 2.2% hadi 3.5%), dizeli (kutoka 27.4 hadi% 33.1%); petroli (kutoka 3.7% hadi 4.7%), ada za shule (kutoka 0.7% hadi 2.9%) na huduma ya malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kutoka 0.9% hadi 3.8%).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live