Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC yazindua mkopo wa bima unaoanzia Sh1 milioni

Mon, 23 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua mkopo wa bima unaoanzia Sh1 milioni ukiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi. 

Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru amesema mkopo huo utaanzia Sh1 milioni hadi Sh300 milioni.

Amesema mkopo wa bima wa NBC ni maalumu kwa ajili ya bima za biashara zote zikiwemo magari, bidhaa zilizo safarini, majanga ya moto, ujambazi, hatari za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.

 “Mtu yoyote mwenye mahitaji ya bima akiwa na rasilimali zozote kama vile nyumba ana sifa ya kupata mkopo huu bila kuwa na dhamana yoyote.”

 “Utalipia miezi miwili ya bima yako NBC na benki tutalipia miezi 10 inayobaki kwa wakala kwa  niaba  yako, wewe utailipa benki kila mwezi kidogo kidogo. Mkopo huu una riba ndogo kuliko mikopo yote inayotolewa na benki,” amesema  Ndunguru.

Mkurugenzi huyo amesema uamuzi wa kuanzisha huduma hiyo inayowalenga wafanyabiashara umetokana na kasi ya utendaji wa serikali ikiwemo kuondoa kero zilizokuwa zikiizorotesha sekta ya uchukuzi nchini.

Pia Soma

Advertisement
Awali, akifungua mkutano huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Isack Kamwelwe ameipongeza NBC kutokana na juhudi inazofanya za kuinua sekta ya biashara ndogo na za  kati.

Kamwewle alitolea mfano hivi karibuni benki hiyo ilisaini makubaliano na Shirika la Posta Tanzania  kwa ajili ya kuweka ofisi kwenye kila tawi la shirika hilo lililopo nchini

Chanzo: mwananchi.co.tz