Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC yatoa mafunzo nidhamu ya fedha

FEDHA WEB NBC yatoa mafunzo nidhamu ya fedha

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wametakiwa kuweka utamaduni wa kujiwekea akiba, kubuni mawazo ya biashara pamoja na kutambua namna ya kutumia taasisi za kifedha kujijenga kiuchumi.

Hayo yamebainishwa Jumamosi Novemba 18, 2023 wakati wa semina masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea utamaduni wa uwekaji wa akiba kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza iliyotolewa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkuu wa Uendeshaji NBC, Alelio Lowassa alisema ni muhimu kuwajengea ufahamu na ujuzi wa kifedha vijana hao wakiwemo wale wanaotarajia kuhitimu elimu ya sekondari na kujiunga elimu ya juu na wale watakaojiri.

“Elimu ya fedha kwa wanafunzi ni muhimu kwa sababu inawawezesha kuelewa mapema jinsi ya kutunza na kuendesha fedha zao, kubuni, kufuata bajeti, na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha,”alisema Lowassa.

Alisema semina hiyo pia, itawafundisha umuhimu wa akiba, uwekezaji, na matumizi sahihi ya mikopo.

“Tunaamini hawa ndio wajasiriamali, wawekezaji na maofisa wa kesho hivyo ni vema kuanza kuwaandaa mapema ili waweze kujua namna ya kutumia taasisi za fedha katika kujikwamua’’

“Hatua hii ni mwendelezo wa jitihada zetu kwenye elimu ambapo kupitia mpango wetu wa wajibika tunatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 1,000 wa vyuo vya ufundi (VETA) hapa nchini,’’ aliswsema.

Hata hivyo Lowassa alisema ukosefu wa elimu ya fedha na ujasiriamali imekuwa ikisababisha baadhi yao wanapohitimu shule kushindwa kwenda sambamba kasi ya uchumi kwenye jamii zao hivyo hujikuta kwenye dimbwi la umaskini hasa pale wanapokosa ajira.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Mavumba alisema elimu hiyo itawasaidia wanafunzi hususani wale wanaotarajia kuhitimu kuwa na elimu ya kujiwekea akiba, kujijenga kijasiriamali hata pale watakaposhindwa kuendelea na elimu ya juu zaidi.

“Elimu hii ni muhimu sana, ni bahati mbaya tu sio wanafunzi wote wamekuwa wakiipata. Wanafunzi wanaohitimu sio wote wanaofanikiwa kupata ajira bali wapo wengi ambao wanaamua kujiajiri wao wenyewe inapotokea hivyo elimu ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya fedha inaweza kuwa na msaada zaidi kwao,”alisema

“Hata wale wanaoendelea na elimu ya juu elimu hii huwasaidia sana kujiwekea akiba na kutumia vizuri fedha wanazopewa na Serikali kama mikopo ya kujikimu huko vyuoni,”alisema Mavumba.

Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzao, wanafunzi Siti Omary na Erick Massawe waaliishukuru Benki ya NBC kwa kutoa mafunzo hayo wakiahidi kuyafanyia kazi hususani kwenye eneo la kujiwekea akiba.

Mbali na Lowassa walioshiriki kwenye mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa NBC, Salama Mussa, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Mahesabu, Fulgence Shiraji pamoja na maofisa wengine waandamizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live