Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC yatia mguu sherehe za Nane Nane

0dc17b5928bdb165e228147bf90892f6 NBC yatia mguu sherehe za Nane Nane

Tue, 4 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WADAU mbalimbali wa kilimo wanaoshiriki na kutembelea Maonesho ya Kilimo maarufu Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, wameonesha kuvutiwa na huduma mpya ya ‘NBC Shambani’ ambayo imebuniwa mahususi kwenda sambamba na mahitaji ya huduma za kifedha za wadau hao.

Akifafanua kuhusu huduma hiyo mpya, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati kutoka benki hiyo, Raymond Urassa alisema imelenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

“Lengo hasa la huduma hii ya ‘NBC Shambani’ ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS (Chama cha Ushirika cha Wakulima) na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.

Mbali na kuwawezesha wakulima hao kutunza fedha zao kwa urahisi, Urassa alizitaja baadhi ya faida za huduma hiyo kwa mkulima mmoja mmoja kuwa ni pamoja na mkulima kupata faida kwa salio la akiba linalozidi Sh 100,000 na kuendelea huku pia kukiwa hakuna makato ya kila mwezi.

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bila ada ya uendeshaji wa akaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wa kulipa wakulima wenye akaunti NBC,’’ alifafanua.

Wakizungumzia huduma hiyo, baadhi ya wadau wa kilimo walisema imekuja wakati mwafaka kwa kuwa kwa sasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo ambayo ustawi wake kwa kiasi kikubwa unategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinakwenda sambamba na mahitaji wa wadau hao.

“Nimeona kupitia huduma hii mkulima anaweza kuweka na kutoa kiasi chochote cha fedha tena kwa wakati wowote.

Huo ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimo tunahitaji ili kufanikisha miamala yetu wakati wowote hususani tunapofanya manunuzi ya pembejeo za kilimo au kuhifadhi fedha baada ya kufanya biashara,’’ alisema Emmanuel Rutatora ambaye ni mkulima kutoka wilaya ya Rorya.

Chanzo: habarileo.co.tz