Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC kuwekeza sekta ya kilimo

Bc0522606a712b54f1204cfd208b9850 NBC kuwekeza sekta ya kilimo

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Biashara ya NBC imejizatiti katika uwekezaji wa sekta ya Kilimo na kuwataka wakulima kuendelea kuwaamini kwenye utoaji wa huduma za kifedha.

NBC imekutana na wateja wao wakubwa na wawekezaji ili kujadiliana masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, NBC imewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuwaamini na kuendelea kutumia benki hiyo inayomsikiliza mteja.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wafanyabiashara wakubwa na Wawekezaji, James Metaron amesema wanafuraha kuona wateja wao ambao wameshirikiana nao katika huduma za kibenki kwa takribani miaka 20 wanaendelea kunufaika kibiashara.

Amesema, benki ya NBC imejikita zaidi katika kuhudumia wateja wote hususani wakulima kwa kuwawezeza kuwaamini na kupata fedha za kununua mazao kutoka kwa vyama vya ushirika, kuandaa shamba na mitaji ya biashara.

“Tunatoa huduma za kifedha kwa wateja wakubwa, kwa upande wa Kilimo tumekuwa tunawasaidia katika kununua mazao kutoka kwa vyama vya ushirika na muda mwingine tunampatia mteja fedha kwa ajili ya kuandaa shamba lake kabla ya kulima,”amesema

Aidha, amesema NBC imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Kilimo kinakua na kupitia benki yao inawahamasisha wateja wadogo na wakubwa kujiunga kutokana na uzoefu mkubwa waliokuwa nao.

“Tunafanya biashara katika sekta zote ila tumejikita zaidi kwenye kilimo ili kusapoti wateja wetu na hata kwa wafanyabiashara wakubwa,”amesema na kuongeza

“Kwa mwaka 2022 benki ya NBC imejizatiti kwa kuwekeza fedha nyingi takribani Bilion 100 ili kuwasaidia wakulima kununua na kusafirisha mazao ndani na nje ya nchi,”

Naye Keneth Woiso ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Woiso inayoshughulika na masuala ya kutengeneza bidhaa asilia za ngozi amesema akaunti yake ya NBC ina umri wa kijana.

Amesema katika kipindi chote NBC wamekuwa na msaada mkubwa kwao na wameweza kushirikiana vizuri pindi anapokuwa amekwama kwenye masuala ya kibiashara kupitia kampuni yake ya Woiso.

Aidha, ameishukuru NBC kwa kazi na jitihada wanazofanya kwa wajasiriamali wakubwa na wadogo pindi wanapotaka huduma za kifedha kama vile mkopo na elimu ya biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live