Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC kuunga mkono Mamlaka za Serikali za Mitaa

Nbc Serikali Ya Mitaa NBC kuunga mkono Mamlaka za Serikali za Mitaa

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) katika kuwawezesha na kukuza maendeleo endelevu kwa manufaa ya jamii.

Azma hiyo ya benki ya NBC imetangazwa na Mkurugenzi wa wateja wakubwa na Shughuli za Serikali wa NBC , Bw James Meitaron wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 38 wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika Zanzibar. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa mkutano huo uliozinduliwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza kwenye mkutano huo Bw Meitoron aliwasilisha pongezi za benki hiyo iliyoonesha kukubaliana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na mamlaka za mitaa katika kuendesha maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania. Alisisitiza ahadi ya NBC katika kutoa suluhisho za kibenki zilizokusudiwa kukidhi mahitaji ya mamlaka hizo.

“Mchango mkubwa wa NBC katika uchumi wa taifa dhahiri ambapo takriban Sh. 66.5 bilioni zilipelekwa katika hazina ya taifa pekee mwaka 2023. Ni fahari kwetu kuwa sehemu muhimu ya safari ya maendeleo ya Tanzania na tutaebdelea kusaidia mamlaka za serikali za mitaa na jamii kwa ujumla,’’ alibainisha Bw Meitoron.

Kwa mujibu wa Meitaron, benki hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa njia ya kielektroniki zilizoundwa kwa ajili ya kuboresha ukusanyaji mapato na mchakato wa malipo kwa Serikali na Halmashauri za Miji. Huduma hizo ni pamoja na huduma ya malipo mbalimbali kwa serikali kupitia mfumo wa yaani GePG, NBC Wakala, mashine za POS, na huduma ya Benki kupitia Simu na Intaneti ambazo zinasaidia kuongeza ufanisi na uwazi katika masuala ya kifedha.

Akisisitiza dhamira ya benki hiyo katika kutoa mikopo mikubwa, Meitaron alitolea mifano mkopo ya dola milioni 200 kwa Serikali ya Zanzibar na mpango wa fedha ya dhamana ya miji. Alikaribisha taasisi za serikali zinazohitaji uwezeshaji wa kifedha kwa miradi muhimu, akisisitiza utaalamu na uwezo wa NBC katika kurahisisha jitihada hizo.

Meitaron amezihakikishia mamlaka hizo kuwa benki hiyo iko tayari kuzihudumia mahitaji yao ya kifedha. 11 hours ago

Chanzo: www.tanzaniaweb.live