Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NBC Yshikilia Tuzo ya Taasisi za Fedha

TROPHY 4?fit=700%2C467&ssl=1 NBC Yshikilia Tuzo ya Taasisi za Fedha

Thu, 15 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

NBC Yshikilia Tuzo ya Taasisi za Fedha July 15, 2021 by Global Publishers



Makamu wa pili waRais Zanzibar Mh Hemed Suleiman Abdulla (wa pili kushoto) akipata maelezokuhusu huduma za Benki ya NBC kutoka kwa Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenkikutoka Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje (kulia) wakati alipotembelea banda labenki hiyo kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasabayaliyohitimishwa jijini Dar es Salaam jana. Wanaofuatilia maelezo hayo pia nipamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (katikati) naMkurugenzi wa Tantrade balozi Mteule Edwin Rutageruka (kushoto). Benki yaNBC ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa Maonesho hayo.

Dar es Salaam. Benki ya NBC nchini Tanzania, imeendelea kuwa kinara kwa mara ya nnemfululizo katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaamkwa kutwaa tuzo mbalimbali ikwemo ya ushindi wa kwanza katika kundi la taasisiza Fedha zilizoshiriki maonesho hayo.

Pamoja na kuwamdhamini mkuu wa Maonesho hayo benki hiyo ilikuwa mstari wa mbele katikakufanikisha ushiriki wa wadau wake mbalimbali katika maonesho hayo wakiwemowajasiriamali, sambamba na kudhamini Kliniki ya biashara iliyoandaliwa kwaushirikiano Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Mkuu wa Kitengo chaMauzo kwa wateja binafsi Benki ya NBC Bw Abel Kaseko akionyesha tuzo ya ushindibaada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za Fedha kwa mara ya nne mfululizo katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaDar es Salaam, yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijiniDar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Makamu wa pili wa Rais ZanzibarMh Hemed Suleiman Abdulla (wa pili kulia – meza kuu) na Waziri wa Viwanda naBiashara Prof. Kitila Mkumbo (kushoto –meza kuu)

Akizungumza kwenyehafla ya ufungaji wa maonesho hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwawateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru alisema ushirikiwa benki hiyo kwenye maonesho hayo umekuwa na tija kubwa kwa kuwa wamepatanafasi ya kuhudumia wateja wao sambamba kufungua fursa mpya za ushirikiano nataasisi mbalimbali likiwemo Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).



Wafanyakazi wabenki ya NBC wakijipongeza baada ya kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo zaubunifu, kutoa huduma na bidhaa bora kwenye maonesho ya Sabasaba.

“Mbali nakushirikiana na taasisi zaidi ya 16 katika kufanikisha kliniki ya biasharakwenye maonesho haya, tumefanikiwa kufungua milango na taasisi nyinginezinazohudumia wajasiriamali na wafanyabiashara wanaochipukia ikiwemo SIDO ilituweze kuona namna ambavyo tunaweza kuunganisha nguvu ili kwa pamojatuwahudumie wadau hao muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara,’’alisema.



Aliongezakuwa wakiwa kwenye maonesho hayo benki hiyo ilipata fursa ya kupokea wagenimbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Makamu waRais Dk Phillip Mpango aliezindua maonesho hayo, mawaziri mbalimbalipamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh Hemed Suleimani Abdulla ambaopia waliiopongeza ipongeza benki hiyo kwa namna inavyoshiriki kuwasaidiawafanyabiashara nchini.



Muonekano wa tuzohizo!

“Kama benkitumejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba tunayafanyia kazi maoni yoteyaliyotolewa na viongozi waandamizi wa serikali pamoja na wateja wetuwaliotutembela lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba tunakusanya maoniyatayatuwezesha kubuni huduma zinazoendana na matarajio yao,’’



Maofisa waandamiziwa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa watejawadogo na wa kati wa benki hiyo, Bw Elvis Ndunguru (Katikati) wakipata maelezo kuhusu bidhaa zinazozalishwana Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kutoka kwa mtaalamu wa mitambo waSIDO- Kilimajaro Bw Boniventure Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Meneja Masoko SIDO Makao Makuu Bi Lilian Massawe (kushoto) wakati maofisa hao walipotembeleabanda la SIDO lililopo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar esSalaam, yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar esSalaam.

“Benki ya NBCtumeendelea kuwa karibu na wafanyabiashara wa kati (SMEs) na ndio maanatumezidi kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji yao kama vile mikopo ya biladhamana kwa wazabuni na wasambazaji wa bidhaa, huduma za kidigitali zinazookoamuda pamoja na gharama nafuu zaidi za uendeshaji ili kuongeza tija kwenyebiashara zao,’’ alisema.



Mkurugenzi waKitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NBC, Bw ElvisNdunguru (Kushoto) akipokea zawadi yabidhaa za chakula kutoka kwa mmoja wajasiriamali wa bidhaa za kusindikwa BiFlora Sumaye ikiwa ni ishara ya shukrani kutoka kwa mjasiriamali huyo kwenda benkiya NBC baada ya benki hiyo kumuwezesha na kudhamini ushiriki wake kwenyemaonesho hayo.

Akizungumziakuhusiana na ushirikiano mpya baina ya benki hiyo na taasisi yake, MkurugenziMkuu wa SIDO Mhand. Prof. Sylvester Mpanduji aliishukuru benki hiyo kwakufungua milango ya kimahusiano na taasisi hiyo huku akibainisha kuwainaonyesha wazi nia ya benki hiyo kuleta mapinduzi ya kihuduma kwa kusaidiasekta ya viwanda na biashara.



Mkurugenzi waKitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NBC, Bw ElvisNdunguru (Kushoto) pamoja na Mkurugenziwa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bi. Neema Rose Singowakiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa kitanzaniawalipotembelea banda la SIDO kwenye maonesho hayo.

“Ushirikiano huumpya na benki ya NBC unadhihirisha nia ya benki hii katika kuinua na kuwasaidiawafanyabiashara wadogo na wa kati. SIDO tunakaribisha vyema mahusiano hayamapya na tupo tayari kushirikiana na benki kwa mustakabari mzima wa ustawi wasekta ya viwanda vidogo na wafanyabiashara nchini,’’ alisema.

Share this:TweetWhatsApp Related
Chanzo: globalpublishers.co.tz