Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NARCO toeni maeneo kwa wafugaji

Ee9f21092cac09116a4036849cd311af NARCO toeni maeneo kwa wafugaji

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS John Magufuli amepigilia msumari wa mwisho kwa kuitka Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO), kutoa maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa wafugaji.

Rais Magufuli alisema kuna maeneo ambayo hayatumiki na ndio maana mifugo haiongezeki hivyo wapatiwe wafugaji.

“Natambua NARCO tuna maeneo mengi lakini hatuyatumii ipasavyo, nafahamu Kongwe kuna ng’ombe 800 wana mimba, lakini hawaongezeki, wafugaji wa kawaida ng’ombe wao wanaongezeka, hata wa kwangu wanaongezekana, ila nyie hawaongezeki sasa toeni hayo maeneo kwa wafugaji,” alisema Magufuli.

Alisema wafugaji wapewe maeneo hayo kwa kukodishwa na gharama nafuu na kwamba Narco wafikirie faida watakayoipata mbele.

Pia Rais Magufuli aliwaomba wananchi kuwekeza kwenye sekta ya mifugo na kwamba mwekezaji sio lazima atoke nje ya nchi.

Kauli ya Magufuli imekuja baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki baada ya Januari 14 kutoa siku 10 zinazoisha Jumamosi ijayo Januari 23 kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao.

Chanzo: habarileo.co.tz