MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, , amesema ifikapo kesho ya Oktoba 31, 2021, ndiyo mwisho wa watu kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa kutokana na muda wa siku 12 alizoongeza kufikia kikomo.
Amesema wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa hususani Kariakoo, kufika soko la Machinga Complex kwa ajili ya kupatiwa nafasi kutokana na soko hilo kusaliwa na nafasi 2,400 za wafanyabiashara.
Makalla amesema hayo alipotembelea soko hilo na kueleza kuwa hadi sasa zaidi ya wafanyabiashara 2,200 wamepatiwa maeneo ya kufanyia biashara na wanafurahia na biashara zinakwenda vizuri sokoni hapo.
Aidha Makalla amesema Serikali imedhamiria kutatua changamoto zote za kibiashara kwenye maeneo walipopelekwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuelekeza LATRA kufikisha huduma ya usafiri wa daladala kwenye maeneo hayo ili kuchochea biashara.