Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi alia na changamoto mahitaji ya chakula

When And How To Plant Corn Seed Outdoors 920x425 1 Mwinyi alia na changamoto mahitaji ya chakula

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, amesema Dunia imekabiliwa na changamoto ya kutojitosheleza kwa mahitaji ya chakula kutokana na ongezeko la idadi ya watu na mabadiliko ya tabia nchi yaliyoathiri uzalishaji.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Desemba 27, 2022 katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwelewa viongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa Kikwajuni, Zanzibar.

Amesema, idadi ya watu Barani Afrika ikiwemo Tanzania na Zanzibar inategemewa kuongezeka maradufu ifikapo 2050 na kwamba hali hiyo itasababisha usalama wa chakula kuwa na changamoto iwapo hatua sahihi hazitachukuliwa mapema, ili kuzuia hali hiyo isiwe janga.

Rais Mwinyi ameongeza kuwa, matumizi ya biteknoloji ya kisasa ni elimu inayowezesha kufanyika mabadiliko ya vijinasaba (DNA) kwa kuvumbua mambo mbalimbali nyanja za Afya, Uchumi wa bluu, Kilimo, Ufugaji, Mazingira na bidhaa za viwandanina kwamba iwapo itatumika kwa usahihi inaweza kuleta maendeleo endelevu kwa haraka.

Akiwasililisha mada kuhusu Bioteknolojia ya Kisasa, Matumizi, Fursa, Faida na changamoto zake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Aly Mahadhy amesema kuwepo kwa kasi ya ongezoke la idadi ya watu, mabadiliko ya tabia nchi na ardhi kuliwa na bahari kutasababisha kukosekana kwa eneo la kilimo na hivyo kuleta uhaba wa chakula.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwaza wa Rais Zanzibar, Dkt. Omar Dadi Shajak, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kufanya tathmini ya masuala yanayohusu matumizi ya teknolojia ya kisasa na kusaidia Zanzibar katika uandaaji wa sera na sheria ili kuweka muongozo sahihi

Chanzo: dar24.com