Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinyi aanika maboresho mazingira ya biashara

Mwinyi Pic Mwinyi aanika maboresho mazingira ya biashara

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Tanzania imechukua hatua kadhaa kuboresha mazingira ya biashara nchini humo.

Rais Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara, wawekezaji wa kitanzania na wadau wa Bandari za Tanzania jijini Bunjubura nchini Burubdi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea leo Ijumaa Julai Mosi, 2022 na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilary, hatua hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa kituo cha pamoja mpakani kati ya Kobero (Tanzania) na Kabanga (Burundi) kuondoa usumbufu wa kuruhusu biashara kufanyika kwa haraka.

“Katika kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, mifumo ya tehama katika bandari hiyo imeimarishwa ili kurahisisha mchakato wa uondoaji wa shehana na kuwezesha wateja kuhakiki stakabadhi zao tozo za bandari,” amesema

Amewahakikishia wawekezaji na wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma zinazotolewa na bandari zote za Tanzania.

Amesema bandari ya Dar es Salaam imeboreshwa kwa kujengwa gati mpya maalumu kwa meli zinazobeba magari pamoja na eneo maalumu la kuegesha magari 6000 kwa wakati mmoja.

Kuhusu usafirishaji wa mizigo kwa gharama nafuu, Rais Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania itaboresha Shirika la Reli (TRC), ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na shehena.

“Serikali itaondoa changamoto zitakazojitokeza kwa lengo la kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Burundi," amesema

Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza Zanzibar katika sekta za utalii, mafuta na gesi, uvuvi na kilimo cha mwani kupitia sera ya uchumi wa bluu.

Rais Mwinyi yupo nchini Burundi akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru Burundi zinazofanyika leo Julai Mosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live