Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Mufuruki kuagwa kwa saa sita kesho

87832 Ratiba+pic Mwili wa Mufuruki kuagwa kwa saa sita kesho

Fri, 13 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kuanzia Saa 1:30 kesho asubuhi hadi saa 6:00 adhuhuri, wananchi watauaga mwili wa bilionea Ali Mufuruki aliyefariki Jumamosi iliyopita nchini Afrika Kusini.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya msiba wa bilionea huyo ambaye mwaka 2012 utajiri wake ulikadiriwa kuwa Dola 110 milioni za Marekani sawa na Sh176 bilioni kwa wakati huo Dola moja ikiwa sawa na Sh1,600.

Ingawa mwakilishi wa Serikali bado hajajulikana, salamu za buriani zinatarajiwa kuongozwa na Balozi Ali Mpungwe atakayesoma wasifu wa marehemu huku Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakurugenzi wa kampuni nchini (CEO Roundtable), Sanjay Rughan akiiwakilisha sekta binafsi.

Dua ya kumuombea marehemu itaongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum, Sheikh huyo pia ataongoza Mawaidha huku Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai atatoa salamu kwa niaba ya vyombo vya habari.

Waombolezaji watakaojumuisha wageni, viongozi na wanafamilia, wataruhusiwa kuingia katika ukumbi wa JNICC kuanzia Saa 1:30 asubuhi kabla mwili haujaondolewa ukumbini hapo kati ya saa 5:50 asubuhi na saa 6:00 kamili adhuhuri.

Mwili utawasili ukumbini hapo saa 3:00 asubuhi kutoka Msikiti wa Mmaamur uliopo Upanga ili kuruhusu ratiba iendelee.

Kabla watu hawajaondoka ukumbini hapo, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Lindam Group, Zuhura Muro atatoa neno la faraja kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Mwili wa Mufuruki tayari umeshawasili jioni ya leo Jumatatu Desemba 9, 2019, baada ya kupokelewa  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), unapelekwa nyumbani kwake Kunduchi na baadaye utapelekwa kuhifadhiwa msikitini.

Chanzo: mwananchi.co.tz