Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwijage: Acheni urasimu nisitumbuliwe

10798 Mwjga+pic.png TanzaniaWeb

Thu, 5 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ataka kila mamlaka isimamie jukumu lake kabla hazijashughulikiwa

Dar es Salaam. Siku moja baada ya kuenguliwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezitaka mamlaka za biashara kuacha urasimu kwa wafanyabiashara ili asitumbuliwe.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua kliniki ya biashara inayolenga kutatua changamoto za kibiashara zinazowakabili wafanyabiashara na kukuza maendeleo ya viwanda na uwekezaji kwa wafanyabiashara wazawa.

“Ninyi mamlaka na sisi, sote tupo katika mtumbwi mmoja akizama mmoja na mimi nitazama,” alisema Mwijage.

Alifafanua kuwa umefika wakati wa kutumia kliniki ya biashara huku kila mmoja akisimamia jukumu lake ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafanikiwa na kukuza sekta ya viwanda na biashara.

“Tunakuja na mpango wa mawasiliano ili uje ‘ku-support’ hii kliniki ya biashara kusudi tuzungunze na wananchi na mamlaka ziwe mwalimu na siyo kituo cha polisi, ziwe makocha. Lakini Rais (John Magufuli) anasema muende na sura ya ubinadamu, unapowafuata wafanyabiashara uwe na sura ya binadamu, Rais kasema haya mchana hamjayasikia?” Alihoji Mwijage.

Alisema ikitokea mamlaka moja imefanya vibaya hata kama nyingine itafanya vizuri, wote wataonekana wabaya.

“Ikitokea mamlaka moja inafanya vibaya tuambizane, tusifurahie kuona inasemwa, kibao kinaweza kubadilika ukatumbuliwa,” alisema Mwijage.

Alishauri kila mamlaka isimamie jukumu lake kabla hazijashughulikiwa.

“Tunataka kusiwapo na kesi za kuanzisha biashara kisha inakufa,” alisema Mwijage.

Pia, alizitaka mamlaka hizo kutoa huduma za haraka kwa wafanyabiashara wanaotaka kujenga viwanda na kuwekeza washughulikiwe haraka.

Chanzo: mwananchi.co.tz