Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigulu: Kigezo cha VAT Sh200 milioni

Efdpic Data Mwigulu: Kigezo cha VAT Sh200 milioni

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara kwa kuamua kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Sura ya 148 kuongeza Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka Sh100 milioni hadi Sh200 milioni.

Hatua hiyo imetangazwa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ameyasema hayo bungeni Dodoma leo Alhamisi ya Juni 15, 2023 wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/24.

“Serikali itaendelea kuongeza kima husika hadi kufikia Sh500 milioni ili kuepusha athari za kimapato zinazoweza kujitokeza,” amesema.

Lengo la hatua hiyo, amesema ni kuongeza ufanisi katika usimamizi wa kodi ya VAT na kuchochea ulipaji kodi wa hiari.

Hata hivyo, amesema hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa Sh75.3 bilioni kwa kuwa walipakodi wenye mauzo ghafi kati ya Sh100 milioni hadi Sh200 milioni ni wengi lakini wamekuwa na madai zaidi kuliko kiasi kinacholipwa kutokana na udanganyifu.

“Walipakodi hawa wataacha kudai Serikali kodi itokanayo na manunuzi yao, sambamba na kupunguza gharama za usimamizi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live