Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigulu: Deni la Taifa limefikia Sh tril 91, tutaendelea kukopa

Mwigulu Pesa Mwigulu Nchemba

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema deni la Taifa liliongezeka na kufikia Tsh trilioni 91, lakini hiyo haiifanyi Serikali kushindwa kukopa ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.

“Deni letu ni TZS trilioni 91, bado tunakopesheka hatuna deni kubwa ukilinganisha na wengine na hatujaacha patakapoonekana hitaji la mkopo hatuna budi kukopa kuwaletea watanzania maendeleo cha kuzingatia ni mkopo wa mashart nafuu,” amesema Mwigulu Nchemba.

Hadi Oktoba 2022 Deni la Taifa liliongezeka kufikia dola za Marekani milioni 39,006.1 (TZS trilioni 91.03) kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kati ya kiwango hicho, TZS trilioni 64 ni deni la nje, huku deni la ndani likiwa ni TZS trilioni 26.6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live