Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa watuma salamu ahimiza kilimo biashara

E180baed34713ed2bfbd27a518b21037 Mwenyekiti wa watuma salamu ahimiza kilimo biashara

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chama cha Watuma Salamu Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Muzazi amewataka wakulima ambao ni wanachama wa chama hicho, kujikita katika kilimo cha biashara na chakula kwa wakati huu mvua zinapoendelea kunyesha kwa kupanda mbegu bora za kisasa zitakazostahamili na kukomaa kwa haraka.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuwahamasisha wanachama hao kutumia mvua hizo ili waweze kulima na kupanda mbegu bora zinazostahamili ukame na zitakazokomaa kwa haraka ili waweze kupata mavuno ya kutosha ya chakula na biashara.

Alisema badala ya wanachama hao kutumia muda mwingi wa kutumiana salamu ni muhimu pia watumie fursa ya mvua zinazoendelea kunyesha, kujikita kwenye kilimo cha kisasa ikiwa na pamoja na kupanda mbegu bora zitakazokomaa haraka ili waweze kupata mavuno ya kutosha kwa ajili ya biashara na chakula.

Hata hivyo amewataka wanachama hao kuhakikisha kila mzazi na mlezi mwenye mtoto anayestahili kuanza elimu ya shule ya msingi na sekondari anampelekwa kupata haki yake ya kimsingi kwa kuwa hakuna sababu yoyote ambayo itakayowanyima na kusababisha kukosa kusoma.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa soko kuu la Majengo amewashauri wafanyabiashara ndani ya masoko kushirikiana kwa pamoja na watumishi wa halmashauri waliopewa dhamana ya kusimamia uwekaji wa mazingira kwenye masoko katika kupindi hiki mvua zinazoendelea kunyesha.

Alisema baadhi ya masoko yaliyopo ndani ya jiji yaliyo mengi miundombinu yake siyo rafiki kama vile mifereji ya maji machafu, hivyo wafanyabishara wanatakiwa kushirikiana na watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia kwa kuyaweka mazingira kwenye upande wa usafi.

Chanzo: habarileo.co.tz