Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwarobaini biashara ya mbao wapatikana

Mbao Ukindu Mwarobaini biashara ya mbao wapatikana

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dkt.Linda Salekwa ameimaliza changamoto iliyokuwa ikiwakabili wavunaji wa miti katika Wilaya hiyo na kupelekea mpasuko mkubwa ndani ya Umoja wa Wavunaji Sao Hill (UWASA)

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi watakao simamia Umoja wa Wavunaji Sao Hill (UWASA) Dkt.Linda Salekwa amesema mzimu uliokuwa unaitafuna jumuiya hiyo ni kukosekana kwa katiba jambo ambalo amelisimamia mpaka kukamilika kwake ambapo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuingoza jumuiya hiyo kufuata sheria na taratibu zote zilizomo ndani ya katiba hiyo.

Naye Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wavunaji Sao Hill (UWASA) Ndg.Chesco Ng'umbi amesema wataisimamia vyema katiba hiyo sanjari na kukuza kipato kwa wavunaji kwani wengi wao wamekuwa wakikutana na changamoto mbali mbali ikiwemo kuuziwa mali zao.

Kwa upande wa viongozi waliomaliza muda wao wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt.Linda Salekwa kwa kuwa kinara wa kusimamia mchakato mzima wa upatikaji wa katiba huku uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi ukikikiri kuziona changamoto hizo ambazo kwa sasa zimetatuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live