Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanri atangaza vita vishoka wa pembejeo zao la pamba

MwaNRI Mwanri atangaza vita vishoka wa pembejeo zao la pamba

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri ametangaza vita na viongozi wa vyama vya msingi vinavyolima zao hilo waliofanya udanganyifu na kupatiwa pembejeo nyingi ikilinganishwa na ukubwa wa mashamba yao na kisha kwenda kuziuza kwenye maduka ya watu binafsi.

Ameyabainisha hayo kwenye semina ya siku moja kwa maafisa ugani, wawakilishi wa wakulima na watendaji wa kata na vijiji iliyokuwa na lengo la kuhamasisha matumizi sahihi ya viautilifu vya zao la pamba katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Balozi Dkt Batilda Buriani ni mkuu wa mkoa wa Tabora amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huo kufanya msako katika minada na magulio ili kuwabaini watu wanaouza viuatilifu hivyo huku akikemea tabia ya wakulima kuchanganya zao la Pamba na mazao mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live