Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwani ina fursa nyingi kiuchumi

Mwani Mwaniii Mwani ina fursa nyingi kiuchumi

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mariam Mwinyi, ameitaka jamii kujikita zaidi kwenye kilimo cha zao la Mwani, kwani kuna fursa nyingi za kiuchumi na kimaendeleo.

Mariam Mwinyi ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kimataifa unaojadili Mifumo ya Chakula Barani Afrika, katika mada ya nafasi ya Mwanamke kwa sekta ya kilimo na chakula.

Amesema kwa upande wa taasisi ya ZMBF imewawezesha kiuchumi Wanawake wakulima wa Mwani baada ya kuwaweka pamoja na kuwapa mikopo nafuu ili waweze kuendeleza zao hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live