Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi abuni mashine ya kuhesabu sarafu

10ed8ac36c547b79706a73cf9c3e7b65 Mwanafunzi abuni mashine ya kuhesabu sarafu

Sat, 9 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MBUNIFU kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Abdulrahman Mussu, amebuni mashine ya kuchambua na kuhesabu sarafu ya kitanzania, ambayo haipo katika maeneo mengi.

Mussu ambaye pia ni mwanafunzi anayesomea Uhandisi na Usimamizi wa Viwanda, Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro, amesema hayo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea.

Amesema ubunifu huo ameufanya baada ya kufanya tafiti kwa baadhi ya benki, makanisani na kwenye taasisi zenye mikusanyiko na kubaini kuwa wanatumia muda mwingi kuhesabu sarafu kwa kuwa wanatumia mikono, hivyo atakapokamilisha ubunifu huo utakuwa ni msaada mkubwa.

“Kwa mfano mtu ana sarafu ziko kwenye ndoo kuzihesabu kwa usahihi fedha hizo unaweza ukachukua muda mwingi sana na usahihi usipatikane.

“Kwa hiyo ufanisi wa mashine hii itakapokamilika ni kwamba kwenye taasisi ya kibiashara badala ya kuajiri watu wahesabu fedha hii yenyewe itakuwa inahesabu fedha kwa usahihi ulio wa juu na haraka,” amesema.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Kitivo cha Sayansi na Teknolojia Mzumbe, Dk. Morris Daud amesema utafiti huo unalenga kutatua changamoto zinazogusa jamii moja kwa moja.

Amesema Mzumbe wanashirikiana na wanafunzi na wanahakikisha wanakuza vipaji vyao kwa kuwashirikisha katika ubunifu, ili wawe watu wanaoweza kuzalisha katika jamii, lakini wawe mabalozi wazuri baada ya wao kumaliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live