Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamunyange ataka ushirikiano wa wananchi mradi wa maji Pugu

Mradipiic Data Mwenyekiti huyo wa bodi amesema ameridhishwa na kasi ya miradi hiyo

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wanaopitiwa na miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini wametakiwa kutoa ushirikiano ikiwemo kulinda vifaa vinavyotumika wakati ujenzi ili kazi hizo kikamilike kwa wakati.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingiraa Dar es Salaam (Dawasa), Jenerali Davis Mwamunyange alipotembelea miradi ya Pugu Gongo la Mboto pamoja na Mbande Chamazi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Amesema ushirikiano kati ya wananchi na watekelezaji wa miradi hiyo una mchango mkubwa katika kuhakikisha inakamilika kwa wakati pamoja na ulinzi na utunzaji wa vifaa.

“Leo hapa tunaona kuna mabomba yanachimbiwa, si kwamba kazi hii itakamilika leo hivyo lazima mengine yatabaki nje ndiyo hapa suala la ushirikiano linapokuja.

“Wananchi mmekuwa mkitoa ushirikiano tunaomba muundeleze na msaidie kulinda vifaa hivi visisogezwe wala kuibiwa ili kusiwe na sababu ya mradi kuchelewa mpate maji ya uhakika na salama,” amesema Mwamunyange.

Mwenyekiti huyo wa bodi amesema ameridhishwa na kasi ya miradi hiyo akielezwa kufurahishwa kwake na wakazi wa Pugu, Majohe, Bangulo, Chanika na Kinyamwezi kuanza kupata maji safi na salama.

Advertisement Mkazi wa Majohe Veneranda Tarimo ameeleza kuwa kabla ya mradi huo walikuwa wakitegemea maji ya visima na mvua hivyo upatikanaji wa maji hayo umewahakikishia usalama wa afya zao.

“Tumeishi kwa kutegemea maji ya visima kwa muda mrefu, ikinyesha mvua tunashukuru tupate maji ya  kunywa lakini sasa tumeondoka kwenye adha hiyo,” amesema Veneranda.

Akizungumzia mradi wa maji wa Chamazi, Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa Dawasa Shabani Mkwanywe amesema ujenzi umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika rasmi Desemba mwakani.

“Tunatarajia Desemba mwaka ujao utakuwa umekamilika wote ila kabla ya hapo kipande ambacho kitakuwa kimekamilika maji yataunganishwa ili wananchi waanze kupata huduma,”amesema Mkwanywe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live